Siri ya Mtungi - Kwa Televisheni, Kwa Watanzania

Uamuzi wa kutayarisha tamthilia ya kiwango cha juu inayoongea moja kwa moja na watu wa Tanzania na Afrika Mashariki una uwezo wa kuleta mapinduzi ya mtandao wa mawasiliano.

Wakati Media for Development International walipopewa jukumu na Johns Hopkins Bloomberg School of Public Health Center for Communication Programs (JHU•CCP) kwa msaada wa Watu wa Marekani (USAID) kutayarisha tamthilia ya televisheni, ilikuwa ni mwanzo wa jambo kubwa zaidi ya rasilmali fedha iliyokusudiwa.
 

USAID Swahili Johns Hopkins Centre for Communication Programs Media for Development International Tanzania PEPFAR


Tangu ianzishwe mwaka 2006, MFDI imekuwa ni gurudumu la ubunifu hapa Dar es Salaam, ikiipa uhai tasnia ya sanaa na wafanyakazi wake, huku ikiweka alama kwa mawasiliano ya kikweli ya Kitanzania.

Kabla ya ujio wa hii tamthilia, MFDI tayari ilikuwa ikiendesha shughuli nyingine kubwa. Mchezo maarufu wa radio, Wahapahapa, ambao pia ulitayarishwa kwa msaada wa Watu wa Marekani na kurushwa kwa miaka mitatu kwenye radio za Tanzania, ulikuwa msingi wa kukua kwa sanaa hii.

Katika miaka hiyo mamia ya wasanii na wanamuziki walijiunga kwenye gurudumu hilo, ambalo sasa hivi linajulikana kama Studio za Wahapahapa, ili kushiriki katika uumbaji wa maonyesho 156 ya tamthilia hiyo ya muziki redioni. Kutokana na onyesho lile, muziki ulirekodiwa na kusambazwa chini ya kitambulisho cha Wahapahapa. Kulikuwa pia na uzinduzi wa bendi ambayo labda bila kushangaza iliitwa Wahapahapa Band ambayo inaendelea kuwa moja ya bendi maarufu na inayofanikiwa sana hapa Dar es Salaam.

Tamthilia ya ‘Siri ya Mtungi’ imeipeleka MFDI kwenye hatua nyingine.

Sio tu kuwa mradi huu umewapatia mbinu mpya na fursa wasanii, wana muziki na wafanyakazi ambao ndio uti wa mgongo wa huu mtiririko wa maono wa Tanzania, lakini hadithi za hawa wahusika kwenye tamthilia hii ya televisheni zimeopolewa toka kwenye hazina ya watu milioni mia moja na hamsini wa Afrika Mashariki wanaozungumza Kiswahili.  

Na kwa hivyo, ‘Siri ya Mtungi’ ina uwezo wa kuwa kipimo, marejeo na mada katika maisha ya maelfu au hata mamilioni ya Watanzania.

Mkurugenzi wa MFDI Tanzania, John Riber, katika muda wote wa maisha yake ya kutengeneza filamu, kuanzia India na Bangladesh hadi Zimbabwe na Tanzania, hajawahi kupata uzoefu kama huu.

Kwa Riber, tamthilia hii imemruhusu kuunganisha uchawi wa filamu na mahitaji ya maendeleo na nguvu ya elimu.

“Niligundua mapema katika kazi yangu hii kuwa nilichokihitaji kukifanya hasa ilikuwa kutumia nguvu ya filamu kuingilia moja kwa moja mchakato wa maendeleo au mageuzi ya kijamii. Nilitaka kutumia filamu kwa watazamaji kwenye nchi zinazoendelea, kutayarisha filamu kwa maendeleo, kinyume na utengenezaji wa filamu kuhusu maendeleo. Na hivyo ndivyo tunavyokabili kazi zetu zote hapa MFDI.”

Tukiwa na rekodi nzuri ya kutengeneza filamu zinazopendwa Afrika – kama vile Consequences, More Time (Poa Mambo Bado), It’s not easy, Yellow Card na Neria – Lengo la Riber pia limekuwa “kuwafanya watazamaji waguswe na visa”.

Kwa hivyo, Siri ya Mtungi, kama zilivyo filamu zilizotangulia kabla yake, inaangukia kwenye mkumbo wa kuwa na wahusika ambao tayari watu “wanawajua na kuwapenda”.

"Filamu kama Consequences, inayohusu mimba za utotoni, tuliyoitengeneza miaka 25 iliyopita, inaonyeshwa hadi leo. Na hiyo ni kwa sababu inahusu watu tunaowajua. Unaiangalia filamu ile na labda unafikiri: Yule anaweza kuwa mimi."

“Kwa tamthilia kama Siri ya Mtungi, tunafanya kitu kama kile , isipokuwa hii ni kubwa zaidi. Kwa sasa kuna wasanii wengi zaidi na wote wana maisha na hali zinazofurahisha zinazofungamana katika hadithi.”

Kwenye hii tamthilia ya televisheni, wahusika wanakabiliwa na masuala yanayotoa changamoto kwa Watanzania wote. Wanataka kujua namna ya kuyafanya maisha yao kuwa bora. Mara nyingine wanaweza; wakati mwingine wanashindwa au hawajui jinsi ya kufanya.

Kama anavyosema Riber: “Ni kweli tunatengeneza sinema kuhusu maendeleo. Lakini hatuhubiri au kutoa majibu. Masuala katika maisha yetu yamechanganyika. Hakuna majibu rahisi. Na hayo ndiyo yanayounda tamthilia."

“Hatuweza kutoa maamuzi rahisi. Lakini tunaweza kutoa hadithi zinazoleta matumaini, zinazoonyesha kwamba watu hawako peke yao wanapokabili changamoto. Tamthilia hii ya televisheni inapenya ndani ya milango iliyofungwa. Tunaona na kusikia mambo nyeti juu ya mahusiano.”

“Ujasiri ni kipengele kikubwa cha filamu za MFDI,” Anasema Riber. “Na kwenye Siri ya Mtungi utagundua uteuzi unaovutia wa mchanganyiko wa wahusika wanaopambana na maamuzi ya nini cha kufanya katika maisha yao. Wengi wanapata ujasiri wa kusimama kidete ili wasiwe waathirika. Wao ndio kizazi kijacho."

ITV Siri ya Mtungi

Siri ya Mtungi Tafsiri

SYM Star Search