Masharubu

Masharubu

Kuna watu wabaya ambao ungependa uwachukie na wengine ungewachukia moja kwa moja. Masharubu ni karaha. Wakati wengine wanaleta mwanga chumbani, yeye hukijaza kiza. Wengine wanapoufanya ulimwengu pahala salama, yeye kazi yake ni kuwapa mateso wengine – kama alivyofanya kwa binti yake mrembo, Nusura, kuyafanya maisha yake jahanamu. Pesa zimemganda kama kinyesi. Baba mwenye nyumba wa mabanda na mageto, anawanyonya watu maskini wanaomzunguka, bila huruma, akiwatoza kodi kubwa na riba kutokana na mikopo anayowapa. Badala yake anawapatia vibanda vibovu waishi. Yeye na vibaraka wake wanaendesha vitendo vya kijambazi bila hata mkono wa sheria kuwafikia ili kuwaadhibu. Amekaa pale kama bwanyenye kuifilisi jamii. Hakuna wa kuthubutu kumwondoa – hata Duma anayemchukia kama upupu.

ITV Siri ya Mtungi

Siri ya Mtungi Tafsiri

SYM Star Search