Maelezo ya Jumla ya Hadithi

Cheche Mtungi - Siri ya Mtungi“Siri ya Mtungi” ni tamthilia ya televisheni inayofurahisha, inayoonyesha maisha ya Cheche, mpigapicha mwenye bashasha na mmiliki wa Studio ya Kupiga Picha ya Mtungi. Ana mke mrembo, Cheusi, aliyemzalia watoto wawili wenye afya na huku akiwa na ujauzito wa mtoto wa tatu.

Cheche anampenda sana mkewe, lakini mawazo ya kuanzisha biashara mpya na kuwepo ujio wa mtoto mwingine wa tatu yanawapa wakati mgumu. Anajaribu kuwa baba mwema, lakini, kama ni uchawi au bahati tu, anawavutia sana wanawake…na wale makahaba! Cheche pia ana uhusiano wa karibu na mpenzi wake wa shuleni, Tula.

Mzee Kizito Family - Siri ya MtungiKizito, ni baba mkwe wake Cheche, aliyemsaidia kuanzisha biashara yake. Ni mtu anayeheshimika sana katika jamii ya Bagamoyo na kila mara anashughulika na watoto wake Nuru na Matona katika karakana yake ya magari. Pamoja na hayo, Kizito ana watoto wengine wengi aliozaa na wake zake watatu, Farida, Mwanaidi na Vingawaje, aliyefariki hivi karibuni.

Soma Zaidi...

ITV Siri ya Mtungi

Siri ya Mtungi Tafsiri

SYM Star Search